Jumatano, 8 Machi 2017

OFFICIAL AUDIO KUTOKA KWA PRINCE TOUZ "MSAMAHA"

Baada ya kimya kirefu tangu msanii wa miondoko ya Rap, mjini Dodoma Prince Touz kukaa kimya sasa arudi kwa kishindo baada ya kuachia ngoma yake mpya iitwayo "MSAMAHA" iliyo beba ujumbe wa mapenzi wenye kuvutia zaidi na kuonyesha hisia za juu zaidi kwa wale walio katika mahusiano hasa katika kukoseana na kuombana msamaha

 
Prince Touz awaweka tayari mashabiki wake kupokea ngoma nyingine kali kutoka kwake pia akiwahakikishia vitu vizuri zaidi huku akilitaja kundi analoliwakilisha G.O.G Click ambao kwa sasa wanaushirikiano wa karibu na kundi la Rap Nation kuwa wamejipanga vizuri kwa mwaka huu.

Aidha mtayarishaji mkongwe wa muziki mjini Dodoma Magnificent almaaruf BM Touchez aizungumzia nyimbo ya "MSAMAHA" katika jicho la kibiashara pamoja na utofauti wa ujio huu wa Prince Touz kwa kubadilika zaidi hasa kwa maamuzi ya kuimba verse ya kwanza swala ambalo lilileta uzito na ugumu wakati wa kurekodi wimbo wa "MSAMAHA" mbali na hayo mtayarishaji huyo makini katika kazi yake pia alizungumzia juu ya ujio wa wasanii wapya kutoka DomTown Records ambao ngoma zao ziko tayari zinasubiri mda uliopangwa kutoka ufike

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni